Zipo tiba malimbali za maumivu ya goti ikiwemo matumizi ya dawa, upasuaji na tiba za fiziotherapia ambapo kila tiba ina nafasi yake katika kumsaidia mgonjwa wa goti au magoti.
Kwenye makala hii nitajikita zaidi katika kuelezea namna tiba za fiziotherapia zinavyoweza kusaidia katika matibabu ya maumivu ya goti au magoti.
Mtaalam wa fiziotherapia ana mchango mkubwa katika kusaidia kutibu ugonjwa huu ambapo atafanya uchunguzi wa awali kubaini chanzo kinachopelekea maumivu ya goti lako na tiba sahihi itakayokufaa.
Tiba hii ya fiziotherapia inalenga kukupunguzia maumivu na kuongeza ubora wa maisha kwa kuongeza ufanisi wa mwili kikazi. Mtaalamu wa fiziotherapia atafanya yafuatayo kutibu maumivu yako ya goti/magoti:
1. Elimu kwa Mgonjwa
Matibabu ya kwanza kwa mgonjwa yeyote mwenye maumivu ya goti ni elimu juu ya chanzo cha tatizo na namna matibabu yatakavyomsaidia.
Elimu hii inajumuisha ushauri sahihi kutokana na chanzo cha tatizo la mgonjwa hasahasa ushauri juu ya umuhimu wa kupunguza uzito na mtindo sahihi wa maisha na lishe ili kusaidia kuleta ahueni ya maumivi ya goti/magoti mapema.
2. Mazoezi tiba
Mtaalum wa fiziotherapia atatoa mazoezi tiba maalumu yanayolenga kuimarisha misuri iliyodhaifu na kuongeza mjongeo katika goti au magoti ambayo husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza maumivu kwenye goti.
Tafiti zinaeleza kwamba mazoezi yameonyesha kuwa yenye ufanisi katika kudhibiti maumivu na pia kuboresha utendaji-kazi wa mwili.
Mazoezi haya yanapaswa kufanyika, mwanzoni, chini ya uangalizi wa mtaalamu wa tiba ya fiziotherapia na baada ya maelekezo sahihi yanaweza kufanywa nyumbani.
3. Tiba za mikono (manual therapy technique)
Kimsingi tiba hii ya viungo inajumuisha kukanda misuli na uhamaji wa viungo ambapo pia physiotherapist hufanya tiba za mikoni zinazohusisha mjongeo wa maungio na goti (mobilization with movement).
Mijongeo hiyo katika maungio ya goti husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza maumivu ya goti.
4. Matumizi ya vifaa tiba vya kuimarisha goti (braces)
Hii inahusisha utoaji wa vifaa sahihi vinavyoweza kusaidia kuimarisha goti na kupunguza maumivu ya goti. Vifaa hivyo ni pamoja na:
Knee Braces
Braces husaidia kutoa msaada na stability kwa goti, na inaweza kuzuia majeraha. Inapatikana dukani kwetu kwa shillingi 74,000 pekee.

Knee Caps
Zinaweza kusaidia kuzuia maumivu na kuvimba; pia inaweza kutoa msaada kwa goti wakati wa mazoezi au shughuli. Unaweza kuzipata Abite Nyumbani kwa TZS 20,000 pekee.

Pain Plasters
Plasters hizi hutoa msaada wa kupunguza maumivu na kuvimba kwa kupunguza maumivu kwa muda mfupi. Mfano wa plasters za maumivu ni Belladona plasters na Capsicula Plasters.

5. Tiba kwa kutumia vifaa vya umeme (electrotherapy)
Vifaa vya umeme kama transcutaneous electrical nerve stimulation (TENS), Therapeutic ultrasound n.k. husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza maumivu ya goti. Vifaa hivi vinahitaji usimamizi wa karibu wa mtaalam wa fiziotherapia pindi vinapotumika kwa mgonjwa.

6. Tiba kwa baridi (Cryotherapy)
Pia inajulikana kama tiba ya baridi; ni matumizi ya joto la chini katika matibabu ya kimatibabu. Cryotherapy hutumika kutibu aina mbalimbali za uharibifu wa tishu unaojulikana kitaalamu kama vidonda.
7. Tiba kwa maji (Hydrotherapy)
Inajulikana pia kama hydropathy; ni tiba kwa maji. Inahusisha matumizi ya maji kwa ajili ya kupunguza maumivu na matibabu. Madhumuni yake ya kutibu ni kuchochea mzunguko wa damu na kutibu dalili za magonjwa.
Hitimisho
Sababu za maumivu ya goti ni nyingi hivyo zinahitaji umakini wa haraka. Kutambua chanzo cha maumivu ya goti ni hatua ya kwanza kuelekea kupata matibabu sahihi. Mambo kama kuchunguza mabadiliko, kuzingatia usafi wa kila siku, na kufanya mazoezi ni muhimu katika kudumisha afya ya goti.
Ikiwa unakabiliwa na maumivu ya goti, usisite kutafuta msaada wa matibabu ili kuhakikisha usalama na afya yako.
Kumbuka, maumivu ya goti si jambo la kawaida. Ni muhimu kutafuta msaada ili kuelewa chanzo chake na kupata suluhisho la kudumu ili kuendelea na shughuli zako.

Physiotherapist Officer (PTO), passionate about transforming the community through education, research and public health advocacy.
