Goti ni kiungo muhimu sana katika mwili kinachoshiriki katika shughuli mbalimblai ikiwemo kutembea, kukimbia, na katika michezo mbalimbali.
Maumivu ya goti ni tatizo ambalo linaweza kuathiri watu wa rika zote na linaweza kuwa na athari kubwa katika shughuli za kila siku.
Tafiti zinaeleza kwamba asilimia 5% ya wagonjwa wanaoripoti katika vituo vya kutolea huduma za afya za msingi wanasumbuliwa na maumivu ya magoti.
Mabadiliko ya mtindo wa maisha hasa katika nchi zinazoendelea pamoja na nchi zenye uchumi wa kati, kama Tanzania, yanasababisha kwa kiasi kikubwa ongezeko la idadi ya wahanga wa tatizo hili.
Nini sababu za maumivu ya goti?
Sababu za maumivu ya goti ni nyingi na zinahitaji umakini wa haraka. Kutambua chanzo cha maumivu ya goti ni hatua ya kwanza kuelekea kupata matibabu sahihi. Katika makala hii nitaeleza sababu 7 zinazopelekea au kusababisha maumivu ya goti/magoti.
1. Homa yabisi (arthritis)
Homa yabisi ni moja ya sababu kuu za maumivu ya goti kwa idadi kubwa ya watu. Ni ugonjwa unaohusishwa na uvimbe wa viungo na unaweza kuathiri goti.
Zipo aina tatu za arthritis amabazo ni osteoarthritis, rheumatoid arthritis na post-traumatic arthritis (arthritis baada ya ajali kwenye goti) – hutokea baada ya jeraha la goti, hasa ikiwa gegedu (cartilage) limeharibiwa.

Osteoarthritis inatokana na kuharibika au kulika kwa gegedu ya goti, wakati rheumatoid arthritis ni ugonjwa unaosababishwa na kinga ya mwili kushambulia viungo vinavyounda goti ambao husababisha uvimbe na maumivu makali, kukakamaa na uwezo mdogo wa kusogea goti.
2. Kupasuka kwa Meniscus
Ndani ya goti kuna kipande cha gegedu kinachoitwa meniscus; mojawapo ya majeraha ya kawaida ya goti ni kupasuka kwa meniscus.
Meniscus ni tishu za gegedu zilizoko katikati ya goti zinazosaidia katika kutoa msaada na kupunguza msuguano kati ya mifupa.
Uharibifu wa meniscus unaweza kusababisha maumivu makali ya goti haswa wakati wa kutembea, kukimbia, au kupinda goti. Uharibifu huu unaweza kutokana na ajali au kuzeeka, na mara nyingi husababisha dalili kama uvimbe na kukosa nguvu katika goti.
Dalili za kupasuka kwa meniscus ni kusikia/kuhisi mlio wa “pop” katika goti wakati jeraha linatokea, maumivu ya papo hapo, kuvimba kwa goti pamoja na ugumu wa kunyoosha au kukunja goti.
3. Majeraha ya Ligamenti
Ligament ni tishu zinazoshikilia mifupa pamoja katika kiungo. Uharibifu wa ligaments kama vile ligament ya mbele ya goti au ligament ya nyuma, yaani ACL (anterior cruciate ligament) na PCL (posterior cruciate ligament), unaweza kusababisha maumivu makali ya goti.
Hali hizi mara nyingi hutokea wakati wa michezo ya kujaribu kubadili mwelekeo au kuanguka. Dalili za jeraha la ligamenti ni kusikia/kuhisi mlio wa “pop”, maumivu, kuvimba, uwezo mdogo wa kusogea pamoja na kushindwa kuweka uzito kwenye mguu.
Majeraha haya yanaweza kuhitaji upasuaji au matibabu maalum ili kurekebisha. Matibabu sahihi ni kuona mtaalamu wa afya au daktari husika ili kufuata ushauri wa kitaalamu na matibabu sahihi.
4. Kukakamaa kwa Misuli na Kupungua kwa Nguvu za misuli
Kukakamaa kwa misuli ya juu na chini ya goti na kupungua kwa nguvu ya misuli inayounga mkono goti kunaweza kusababisha maumivu. Hali hizi zinaweza kuhusishwa na kukosekana kwa mazoezi ya kutosha au kuzeeka.
Watu wanaposhindwa kufanya mazoezi, misuli inakuwa dhaifu na huweza kusababisha maumivu ya goti wakati wa kutembea au kufanya kazi za kawaida.
5. Magonjwa ya Tendoni (Tendinitis)
Tendinitis ni hali inayohusisha uvimbe wa tendons, ambao ni tishu zinazounganisha misuli na mifupa. Tendinitis ya goti, inayojulikana kama patellar tendinitis, inaweza kusababisha maumivu katika sehemu ya juu ya goti.
Hali hii mara nyingi inatokea kwa watu wanaoshiriki katika michezo ya kuruka au kukimbia, ambapo matumizi makubwa ya goti yanaweza kusababisha maumivu.
6. Majeraha ya Mifupa na Misuli
Majeraha katika mifupa au misuli ya goti ni miongoni mwa sababu kuu za maumivu. Hali kama vile sprains na strains zinaweza kutokea kutokana na ajali, kuanguka, au kuumia wakati wa michezo.
Sprains zinahusisha uharibifu wa ligaments wakati strains zinahusisha uharibifu wa misuli au tendons. Majeraha haya yanaweza kuleta uvimbe, maumivu, na kupungua kwa uwezo wa kutembea.
Naomba ufanye replacement ya maneno ya “sprains and strains” kwa kutumia Kiswahili.
7. Masuala ya Kihisia (Psychological pain)
Masuala ya kiakili kama vile msongo wa mawazo na wasiwasi yanaweza pia kuathiri maumivu ya goti.
Wakati mtu anapohisi msongo wa mawazo, mwili unaweza kujibu kwa maumivu ya kimwili katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na goti.
Ni muhimu kutambua kwamba maumivu ya goti yanaweza kuwa na uhusiano na hali ya kihisia, na kutafuta msaada wa kitaalamu kunaweza kusaidia katika kutatua matatizo haya.
Ni mambo gani yanayoongeza hatari ya maumivu ya goti/magoti?
Baadhi ya mambo yanaweza kuongeza hatari yako ya kupata matatizo ya goti, ambayo ni pamoja na:
Unene kupita kiasi au uzito wa ziada
Kubeba uzito kupita kiasi huongeza msongo kwenye viungo vya goti na kuongeza hatari ya kupata osteoarthritis.
Uzito uliopitiliza kuanzia kizio cha uzito (body mass index) zaidi ya 25 ni hatari na inapelekea kuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya goti kama Osteoarthritis.
Ukosefu wa unyumbufu au nguvu ya misuli
Nguvu ya misuli husaidia kuimarisha na kulinda viungo vyako, huku unyumbufu wa misuli ukisaidia kuongeza upana wa mwendo wa viungo.hivyo tunashauriwa kufanya mazoezi ili kuepukana na hatari hii.
Michezo inayoathiri magoti
Michezo kama vile kuteleza chini ya mlima (skiing), mpira wa kikapu, na kukimbia inaweza kuongeza hatari ya kuumia goti; pamoja na michezo ya kugusana.
Jeraha la Awali
Kuwa na jeraha la goti hapo awali huongeza uwezekano wa kuumia tena.
Urithi na historia ya familia
Ikiwa unatokea katika familia ambayo ina historia ya kuugua ugonjwa wa magoti kuna hatari pia ya kupata matatizo haya ya maumivu ya magoti. Magonjwa kama osteoarthritis na rheumatoid arthritis kwa kiasi fulani huwa ni ya kurithi kutoka kizazi hadi kizazi.
Mwisho
Zipo tiba malimbali za maumivu ya magoti ikiwemo matumizi ya dawa, upasuaji na tiba za fiziotherapia ambapo kila tiba ina nafasi yake katika kumsaidia mgonjwa wa goti au magoti.
Kwenye makala yangu ijayo nitaelezea kwa kina namna tiba za fiziotherapia zinavyoweza kusaidia katika matibabu ya maumivu ya goti au magoti.

Physiotherapist Officer (PTO), passionate about transforming the community through education, research and public health advocacy.
