Shirika la Afya duniani (WHO) linaelezea ugonjwa sugu kama ugonjwa unaodumu zaidi ya miezi mitatu na kuendelea.
Ugonjwa wa Arthritis ni miongoni mwa magonjwa sugu yanayosumbua sana jamii. Wagonjwa huelezea kupata maumivu makali yanayopelekea washindwe kulala usiku na kufanya shughuli zao za kiila siku.
Baadhi ya dalili za ugonjwa huu ni maumivu makali yanayokuja hasa muda wa kutembea au kutumia kiungo, kukakamaa na kuvimba joint, na kadhalika. Maumivu yake huja wakati wa kutumia kiungo na wakati mwingine baada ya kazi ya siku nzima.
Ugonjwa huu, kwa asilimia 70%, huja kulingana na umri kuongezeka na ni maarufu sana kuanzia miaka 45 na kuendelea.
Wanawake huingia katika hatari ya kupata Arthritis pale hedhi yao inapokoma (menopause) na hivyo kufanya asilimia 75% ya wanawake kuwa katika hatari ya kupata tatizo hili. Wanaume hupata arthritis mara nyingi kuanzia miaka 50 na kuendelea.
Visababishi vingine ni kama ajali, kukaa vibaya kwenye kiti, historia ya kuumia kwenye michezo, maambukizi ya bakteria, pamoja na shida zingine za kibailojia.
Arthritis inatibikaje?
Dawa za maumivu na za kupunguza uvimbe ni moja ya matibabu. Hata hivyo ugonjwa huu, hasa kama mgonjwa ana historia ya ajali au pingili zimelika kutokana na uzee au magonjwa ya joint, unaweza kuhitaji njia mbadala.
Kutokana na kulika kwa viungio (joint), mara nyingi ugonjwa huu huitaji matibabu endelevu ya muda mrefu.
Matibabu endelevu yanahusisha nini?
Moja kati ya kosa kubwa linaloendelea kufanyika katika kutibu maumivu sugu ya joint ni matumizi ya dawa za kumeza au kuchua pekee.
Kwa bahati mbaya, hii imefanya wagonjwa kuendelea kuwa na maumivu muda wote na pia kupata madhara mbalimbali yakiwemo ya figo, moyo na pia ukuta wa tumbo kupata mushkeri (Gastritis) na kupelekea kuzalisha magonjwa mengine.
Matibabu ya Joint (arthritis) yanapaswa kuhusisha mambo makuu matatu:
- Dawa za maumivu: Sio kila mara ila pale maumivu yanapokuwa hayavumiliki.
- Msaada wa ushauri na kisaikolojia: Wagonjwa wa Arthritis huitaji sana msaada wa kisaikolojia pamoja na kuambiwa ukweli juu ya kisababishi cha maumivu makali na pia kuwashauri njia mbalimbali za matibabu ambazo zinaweza kuhusisha upasuaji, mazoezi na kadhalika.
- Huduma ya mazoezi tiba pamoja na vifaa tiba: Njia hii ni moja ya njia bora zaidi za kuwasaidia wagonjwa wa arthritis. Mazoezi tiba (Physiotherapy) ni moja ya hatua kubwa ya matibabu iliyochagizwa zaidi na teknolojia.
Unajua mazoezi ya viungo yanapunguza kabisa maumivu sugu ya joint? Njia hii imethibitishwa na tafiti mbalimbali ambazo zimeonyesha wagonjwa wengi wanaopata mazoezi tiba wana nafuu zaidi kuliko wale wanaotumia dawa peke yake.
Ukiachana na kufanyiwa mazoezi hospitali, bado kuna vifaa mbalimbali unavyoweza kuwa navyo nyumbani na ukaweza kupunguza maumivu kwa kiasi kikubwa sana.
Vifaa kama Heating Pad, Tens Massage Machine, Gell Exercise Ball, Exercise bands, na Gym ball ni miongoni mwa vifaa tiba ambavyo vinasaidia kupunguza maumivu na kupunguza matumizi ya dawa za maumivu kwa asilimia zaidi ya 75%.
Zaidi kwa maumivu ya joint za mgongo matumizi ya viti maalum kama curble chair na mito maalum Kwa ajili ya kupunguza maumivu Kama coccyx pillow yamesaidia Sana kuondoa maumivu.
Baadhi ya wagonjwa hufikia hatua ya kushindwa kutembea vizuri na kuingia katika hatari ya kuanguka na kuvunjika, hawa wanaitaji Fimbo tiba ya kutembelea kwa ajili ya sapoti. Kutofanya hivi hupelekea kutembea wakiwa wamepinda upande mmoja na mwisho wa siku wanaweza kuanguka na kuvunjika au wakaanza kuugua mgongo kutokana na uti wa mgongo kupinda.
Kundi jingine la wagonjwa wenye maumivu makali ya joint hufikia hatua ya kushindwa kuchuchumaa chooni hivyo huitaji viti vya kukalia chooni, mfano commode chairs.
Mwisho
Ugonjwa huu hautibiwi kwa kumeza dawa pekee, unahitaji njia mbadala ya mazoezi ya viungo na vifaa tiba muhimu kwa ajili ya kuongeza ubora.
Abite Nyumbani tunatoa huduma ya vifaa tiba muhimu. Njoo au mlete mgonjwa wako, tumuangalie, tumshauri huduma au vifaa gani atumie ili kumpa auheni. Tunapatikana Sinza Mori, jengo la Azaria Plaza (ofisi namba 14), opposite na Kitambaa Cheupe Lounge.
Kama upo mbali au nje ya Dar es Salaam, unaweza kutupigia simu kwenye namba +255 767 226 702 kwa msaada wowote utakaohitaji.
Pioneering the future of healthcare in Tanzania and East Africa by harnessing the power of technology to revolutionize patient care and improve outcomes.