Mambo matatu ya kuzingatia baada ya Upasuaji

Baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa kama wa uzazi, tumbo, mifupa na kadhalika, mwili wako huwa haubaki kama ulivokuwa.

Mengi huwa yanatokea mfano, ngozi iliyokuwa imefunga hubaki na uwazi; kupoteza kiasi kingi cha maji, damu na seli baddhi; mwili kubaki na uchovu kwa sababu ya dawa za usingizi; na pia maumivu ya kidonda.

Sasa baada ya upasuaji, kama mgonjwa utaruhusiwa kurudi nyumbani baada ya uangalizi wako pale hospitali kuisha. haya ndiyo mambo matatu ya kuzingatia unaporuhusiwa kurudi nyumbani:

1. Fanya mazoezi madogo (Ambulation)

Unapokuwa na maumivu ya kidonda ni rahisi sana kutaka kulala tu bila kuamka au kwenda popote kwa maana ya kupunguza maumivu na pengine kuogopa labda kidonda kitafumuka.

Hali hii ukinzana kabisa na sayansi ya uponaji wa kidonda na pia madhara yanayoweza kutokana na tabia hii ya kulala au kukaa tu (immobility).

Mnamo mwezi October 2018, mtandao wa National Library of Medicine (NLM) wa Marekani ulichapisha utafiti uliofanywa na hospitali moja nchini humo ambapo ilifanya stadi ya wagonjwa 127 waliolazwa katika hospitali hiyo baada ya upasuaji kwanzia mwaka 2014 mpaka 2017.

Katika utafiti huu waligundua kwamba asilimia 50 ya wagonjwa walioanza mazoezi mepesi ndani ya masaa 24 baada ya upasuaji walipona haraka na kuruhusiwa walau ndani ya siku 3.

Wakati kundi la pili wao hawakuanza mazoezi kwa kuogopa maumivu na walijikuta wanachelewa kupona na kubaki mpaka siku 6 hospitali.

Vile vile hata nyumbani, wagonjwa ambao huamka na kukaa kitandani, kufanya matembezi aidha wenyewe au kwa kusaidiwa na watu wao wa karibu kufanya mwendo kadhaa, kusimama, kwenda chooni na kadhalika waliwahi kupona haraka na kuepuka madhara ya operation kama damu kuganda.

Mazoezi ya mapema yana faida gani?

Kwanza, huongeza mzunguko wa damu na hivyo kupeleka chembe muhimu katika kidonda.

Pia huongeza kiasi cha virutubisho na hewa ya oxygen inayoenda kwenye kidonda na hivyo kuharakisha kidonda kupona haraka, Pia husaidia kuimarisha misuli na kupunguza maumivu ya muda mrefu.

Fanya mazoezi yafuatayo

  • Jaribu kuamka mwenyewe na kukaa pembezoni mwa kitanda. Unaweza kusaidiwa kusogea pembezoni mwa kitanda lakini jitahidi kukaa mwenyewe.
  • Zoezi la kunyoosha mikono na miguu ukiwa umelala mfano kuinua miguu juu na chini, au kupandisha na kushusha mikono.
  • Kusimama aidha kwa kusaidiwa au kujikokota mwenyewe; hakikisha kuna msaidizi karibu.
  • Kutembea umbali mfupi, kwa kusaidiwa au mwenyewe, lakini kuwe na mtu karibu.

Muhimu

  • Epuka kutembea peke yako bila msaidizi wa karibu kwasababu kuna hatari ya kuanguka au kuumia
  • Mazoezi yawe ya taratibu na yaongezeke kadiri ya unafuu unapopatikana. Epuka kuanza na mazoezi makubwa, ni hatari kwa kidonda
  • Utafiti unaonyesha hata mazoezi kidogo huleta tofauti kubwa.
  • Kumbuka wakati unajaribu haya Kuna swala la kuskia maumivu Lakini vumilia tu maana zoezi Lina umuhimu wake.

2. Lishe yenye virutubisho muhimu

Baada ya kufanyiwa upasuaji, mwili huwa unahitaji kurudi katika hali yake ya mwanzo.

Kidonda kinahitaji virutubisho ili kupona haraka. Vyakula vyenye vitamini na protini ni muhimu sana kwa uponaji wa haraka.

Vitamini C, Vitamini A na Vitamini B ni muhimu sana kwa ajili ya kupona haraka.

Juice ya machungwa, embe, nanasi, na papai ni muhimu kwenye kuharakisha uponaji wa kidonda.

Nyama na mayai ni muhimu pia kwa ajili ya kukupa protini ya kutosha kujenga mwili inavyopaswa.

Pia mtu mwenye mshono, hasa tumboni, hapaswi kupata choo ngumu kwahiyo vyakula muhimu kwake ni kama maharage, kabeji, mchicha, ndizi bukoba, na maji ya kutosha – hata kama huna kiu.

3. Kidonda kisafishwe kwa wakati

Kidonda mpaka kipone kinatakiwa kusafishwa walau mara mbili kabla ya kutoa nyuzi, na baada ya kutoa nyuzi bado kinaweza kuhitaji kusafishwa mpaka kikauke vizuri.

Ni muhimu kuzingatia hili na kuhakikisha unarudi hospitali kusafisha.

Kama unampango wa kusafisha nyumbani, ni bora kupata kampuni zinazojihusisha na shughuli hizi kama Abite Nyumbani, watakupa nesi wa kukusafisha katika mazingira ya usafi.

Epuka kusafisha kidonda mwenyewe kwani unaweza kusababisha maambukizi ya bakteria na ikawa mtihani kupona.

Hakikisha unapooga haukilowanishi kidonda kwa ajili ya kuepuka nyuzi kuoza (Japo itategemea na maagizo ya daktari kulingana na nyuzi alizotumia)

Usisahau kumeza dawa zako mpaka mwisho wa dozi. Epuka kukatisha dozi yako kwa sababu ya sherehe au kitu chochote, kidonda kikipata maambukizi utasota muda mrefu.

Mwisho

Uponaji wa kidonda hutegemea utimamu wa kinga yako, umri wako, aina ya upasuaji, na ukubwa wa kidonda pia.

Hivyo, kama una magonjwa kama sukari, cancer, Ukimwi, figo, moyo na utapiamlo unaweza kuchelewa kupona. Ni vyema kuelewa hilo na kutilia mkazo hayo mambo matatu.

Huduma hizo unaweza kuzipata nyumbani kwa kupewa mtaalamu wa afya ambaye atakusimamia kwa usahihi zaidi. Wasiliana na Abite Nyumbani kwa ajili ya kufanya booking ya mgonjwa wako atakayeruhusiwa hivi karibuni kutoka hospitali.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *