1. Athari ya kisaikologia (mental trauma)
Mtu aliyepona au kunusurika na ajali huathirika kisaikologia kiasi cha kuogopa hata kupanda gari, na anapopanda gari basi huwa na hofu kubwa sana (phobia).
Jambo hili huweza kuathiri mpaka utendaji wake wa kazi.
2. Maumivu ya viungo
Baada ya ajali, mtu huweza kuvunjika au kupata maumivu/majeraha makubwa ambayo huweza kuchukua muda mrefu kupona na hivyo kupelekea athari za kisaikologia na kiuchumi (kuchelewa kurudi kazini kwa wakati au kutoendelea kabisa na kazi).
3. Ulemavu wa viungo
Hasa kukatika miguu au mikono, kuvunjika mikono/miguu, au kuumia uti wa mgongo na kadhalika.
Hali hizi zinapotokea huwa na madhara makubwa kwa mtu husika, na watu hawa hasa baada ya kutibiwa huhitaji mwendelezo wa matibabu ya muda mrefu nje ya hospitali (home healthcare).
Msaada wa kisaikologia, msaada wa mazoezi ya viungo na msaada wa kusafisha vidonda huwa ni uhitaji wa muda mrefu.
Ukizingatia uoga wanaoupata wa kupanda magari na kadhalika, watu hawa watanufaika zaidi na huduma ya afya nyumbani na utafiti umeonyesha kwamba kutibiwa nyumbani huarakisha uponaji wa mgonjwa.
Mgonjwa hapotezi muda kuwaza gharama za kitanda na usafiri wa kila siku, bali anakuwa na muda wa kupumzika na kupata huduma nzuri ya nyumbani kutoka kwa familia huku akitibiwa, ukizingatia gharama za huduma afya nyumbani huwa ni nafuu sana kulinganisha na mahospitalini.
Pioneering the future of healthcare in Tanzania and East Africa by harnessing the power of technology to revolutionize patient care and improve outcomes.
Niliwahi kushuhudia ajali moja kipindi cha nyuma nikiwa shule sijawahi kusahau ilileta hali ngumu sana kwa majeruhi na ilisababisha kuwe na woga hasa wa kuvuka barabara kipindi hicho ambayo ilipungua tu baada ya muda ila haijaondoka kabisa
Yes, ukipata hali kama hiyo unahitaji msaada wa kisaikologia @Ester.