Daktari kwanini usianzishe huduma ya afya nyumbani?

Ni maneno ya kaka mmoja, Bwana Erick Rutahya, aliyekuwa akimuuguza mke wake mwenye kansa ya titi. Walikuwa wanaishi maeneo ya kimara suka.

Nilikutana naye wakati amekuja kuchukua majibu ya vipimo vya mke wake katika kituo cha afya nlichokuwa nafanya kazi, MCD Hospital.

Baada ya kunielezea hali ya mke wake na jinsi ilivyo changamoto kumsafirisha mpaka Muhimbili na kurudi kwa ajili tu ya kusafisha kidonda na msaada wa choo, tulifkia muafaka kwamba niwe naenda kwake kusaidia atakuwa ananipa malipo kiasi.

Wiki liyofuata nilianza kwenda kwake mara tatu kwa wiki walau kumchoma mkewe sindano za maumivu na kumsafisha. Alifarijika sana na gharama zake za matibabu (pamoja na kumpeleka mkewe muhimbili) zilipungua na wakati mwingine alipotaka kunilipa nilikataa, niliamua nimsaidie tu.

Katika kipindi hiki nilichokua namtibu mama huyu nyumbani kwake niligundua huduma yangu ilisaidia sana watoto na mume wake kubaki nae nyumbani, kumuona kila siku, kucheka nae, kula nae na kumpa msaada muhimu.

Siku moja wakati nikiwa namfanyia usafi mkewe akanambia sentensi moja ambayo ndiyo ilikuwa chachu ya kuanza kuwaza kuja kufanya huduma ya afya nyumbani.

Alinambia hivi…

“Lakini daktari msaada unaonipa ni mkubwa sana, amini kuna watu wengi kama mimi nao wana wagonjwa wao na wanapata shida sana, kwanini usianzishe huduma ya afya nyumbani?”

Niliwaza sana wakati niko njiani kwenye daladala narudi nyumbani, lilitengeneza kitu ndani yangu na kunipa chachu ya kuwasaidia wagonjwa wenye magonjwa sugu kwa kuwapa huduma nyumbani.

Baada ya kama mwezi mmoja, Mr Erick alinitumia ujumbe kwamba mkewe amefariki na kunishukuru kwa huduma niliyotoa kwake.

Hii ilinipa nguvu kuona kwamba kuna jambo tunaweza kufanya kusaidia jamii kwa kutoa huduma bora ya afya nyumbani.

Naiyona Abite Nyumbani ikitimiza hilo lengo.

2 thoughts on “Daktari kwanini usianzishe huduma ya afya nyumbani?”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *