Najua unapenda kufanya mazoezi nyumbani kama mimi au sio? Binafsi nilianza kufanya mazoezi nyumbani kwa sababu kuu tatu.
Kwanza, muda finyu wa kwenda Gym Kila siku. Napenda sana mazoezi lakini kila muda wa Gym ulipofika nilijikuta sina muda kabisa na hivyo kujikuta nakosa hadi wiki mbili mfululizo.
Pili, kiuchumi. Gym nyingi za mjini ni gharama sana hasa ukiwa na uchumi wa wastani. Kulipa elfu 3 kila siku ni changamoto.
Tatu, Gym kuna vishawishi sana hivyo nilijikuta sifikii malengo yanayonipeleka Gym. Ndipo nilipojifunza kufanya mazoezi yangu nyumbani na nikagundua ni maamuzi sahihi sana.
Hivi ndivyo vifaa vitatu vitakavyokusaidia kufanya mazoezi nyumbani kwa ufanisi sana.
- Exercise Band Loops: Hizi ni rubber bands ambazo zinatumika kufanya mazoezi ya viungo. Ukiwa na hizi bands, basi unaweza kufanya mazoezi lukuki ya mikono, miguu, kiuno, mabega, kifua, na kadhalika.

Kutumia bands kunaondoa matumizi ya kubeba vyuma huku ukipata faida zilezile.
Kifaa hiki kina band za ukinzani tofauti tofauti hivyo unaweza kufanya mpaka uzito wa juu kabisa. Kama unapenda kufanya workouts nyumbani, basi hii itakufaa sana.
- Exercise Gym Ball: Huu ni mpira wa maajabu sana. Una msaada mkubwa kuanzia kuondoa maumivu ya viungo mpaka kujenga misuli ya kifua, tumbo, makalio, miguu, mbavu, na kadhalika. Wewe ni mjamzito? Basi Gym ball inakuhusu moja kwa moja. Hukupa uhuru wa kufanya mazoezi ya ukakamavu wakati wa ujauzito wako.

Mpira huu ukiwa nao basi umejikomboa kiafya tayari, unaweza kufanya mazoezi zaidi ya 24 kupitia pira huu.
Kama kweli umeamua kufanya mazoezi nyumbani, basi miliki Gym ball yako.
- Exercise Mat: Huu ni mkeka maalum kwa ajili ya mazoezi nyumbani. Sakafu yenye tyles huwa inateleza hivyo hupelekea kushindwa kufanya mazoezi mengi hasa ukishaanza kutoa jasho; ukiwa na mkeka wa mazoezi basi hautateleza na utafanya mazoezi yako kwa ukubwa unaotakiwa.

Vifaa hivyo vitatu ukiwa navyo basi wewe utakuwa umewekaza kweli katika mazoezi ya nyumbani na itakulipa sana.
Kumbuka: Ukiwa na vifaa vya mazoezi nyumbani unaweza kufanya mazoezi yako muda wowote; iwe asubuhi, mchana, usiku au alfajiri. Hauna mipaka kabisa na hakuna kulipa ada ya mwezi Gym.
Vifaa vyote hapo juu, utavipata dukani kwetu. Tupigie simu kwenye namba +255 767 226 702 kwa ushauri wa afya (bure) na mahitaji ya vifaa tiba vya aina zote.
Tunapatikana Sinza Mori, jengo la Azaria Plaza (ofisi namba 14), opposite na Kitambaa Cheupe Lounge. Karibu sana!

Pioneering the future of healthcare in Tanzania and East Africa by harnessing the power of technology to revolutionize patient care and improve outcomes.
