Jinsi ya kuishi na ugonjwa wa Moyo, kisukari, HIV/UKIMWI, au Kansa baada ya kutoka hospitali

Kumeza dawa zako kila siku na muda ule ule – hii ni ishara ya nidhamu na kukubali ugonjwa

Na mara kwa mara wagonjwa wanao fanya Hivi huwa na matokeo mazuri. Epuka kumeza dawa kadiri unavojiskia na Kutomeza siku kadhaa, hii huuchanganya mwili na kufanya ugonjwa wako kuendelea kukua.

Kuwa na daktari wako wa karibu

Hii husaidia kupata ushauri wa mara kwa mara pamoja na kumtumia vipimo vyako mara kwa mara. Daktari huyu anaweza kukushauri uende hospitali mapema kama atagunda hauko sawa kuliko kusubiria miezi mitatu ndio urudi hospital au clinic.

Kutokuwa na uangalizi wa karibu ndio husababisha ukirudi hospitali unakuta mambo sio sawa.

Fuata maelekezo ya Lishe na mtindo bora wa maisha

Kama umeshauriwa mazoezi, fanya mazoezi. Kama umeambiwa usile chumvi, basi punguza au usitumie kabisa. Kama hutakiwi kuvuta sigara, acha sigara.

Kumbuka unafuu wa magonjwa haya upo zaidi katika nidhamu.

Kubali kwamba unaumwa.

Mfano wa wagonjwa wawili wenye HIV: Mgonjwa anayekubali ugonjwa humeza dawa kwa wakati na huishi muda mrefu bila magonjwa nyemelezi, wakati yule asiyeridhia hali hukataa dawa na kuamua kusali tu na baada ya muda hali huwa mbaya na kufariki mapema.

Hudhuria kliniki kwa muda unaopaswa pamoja na kufanya vipimo mara kwa mara.

Muhimu: Magonjwa haya yanaweza kutibiwa na kufatiliwa nyumbani bila ulazima wa kwenda hospitali mpaka pale ukiwa umezidiwa, endapo ukilipia gharama kidogo kwenye home healthcare services kama Abite Nyumbani, utakua umeongeza ufanisi na uwezekano wa kukaa muda mrefu bila kusumbuliwa na maradhi nyemelezi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *