Sasa Unaweza Kukodisha Kitanda cha Hospitali Ukiwa Dar es Salaam

Ulishawahi kusikia huduma ya kukodisha kitanda?

Mara ya kwanza nasikia huduma hii nilikuwa zangu kitaa natafuta kitanda Cha mdogo wangu aliyekuwa kafanyiwa upasuaji wa nyonga.

Gharama zilikuwa juu na budget ya familia ndogo sana.

Baada ya kuzunguka bila mafanikio ndipo nikaamua kuiyuliza Google kuhusu huduma ya kukodisha. Nilishangaa sana kujua kwamba huduma hii ipo na inatolewa hapa hapa Dar Es Salaam!

Nilipata kitanda kizuri kwa gharama ambayo sikutarajia. Bei ya kununua mtaani niliambiwa ni Milioni moja na nusu (TZS 1.5M) ila niliweza kukikodi kwa shilingi laki 4 (TZS 400,000) tu.

Baada ya kuanza kukitumia nyumbani, wiki mbili na nusu, mgonjwa alifariki kutokana na maradhi mengine yaliyokuwa yanamsumbua.

Hapo ndipo nikajiuliza: Ningekuwa nimekinunua kwa gharama ile kubwa ingekuwaje?

Binafsi nashauri kama mgonjwa wako ni mahututi sana au ni kijana ambaye anaweza kupona mapema, basi ni bora kukodisha kitanda au wheelchair kuliko kuinunua. 

Kama baadaye itaonekana mgonjwa wako si wa kupona leo basi unaweza kuongeza pesa kadhaa ukanunua moja kwa moja.

Kama unataka huduma hii basi wasiliana na Abite Nyumbani (kupitia simu namba 0767 226 702), taasisi inayouza na kukodisha vifaa hivi Tanzania.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *