Mgonjwa anaporuhusiwa kutoka hospitali, lugha huwa ni moja tu: Kanunue wheelchair.
Hii haijalishi una pesa au huna. Haijalishi mgonjwa wako ni wa kuendeshwa siku zote au atapona muda mfupi.

Kwa kawaida, mgonjwa kuanzia miaka 0 mpaka 55 akivunjika mfupa wake, huchukua kati ya wiki 6 mpaka 8 kuunga.
Lakini, wiki mbili baada ya kuvunjika huwa anaweza kutembea mwenyewe.
Kwa maana hiyo anahitaji wheelchair kwa wiki moja au mbili tu, na baada ya hapo haiitaji tena.
Je, kuna ulazima wa kununua kitimwendo moja kwa moja kwa mgonjwa wa namna hii?
Jibu ni: sio lazima kununua.
Kwanini?
Kwa sababu unaweza kukodi.
Kukodi kuna faida nyingi, ikiwemo: Kupunguza gharama zisizo za lazima na kuondoa hali ya kubaki na kifaa kisichotumika na mwishowe kujaza nafasi.
Kiasi unachookoa kinakuwa na matumizi ya kumsaidia mgonjwa apone haraka mfano, kulipia mazoezi tiba.
Una mgonjwa mwenye mahitaji haya?
Unaweza kukodi kutoka Abite Nyumbani.
Wasiliana na Abite Nyumbani, kupitia simu namba +255 767 226 702 au WhatsApp, kwa maelezo zaidi.

Pioneering the future of healthcare in Tanzania and East Africa by harnessing the power of technology to revolutionize patient care and improve outcomes.